Kila idara ni fursa ya kukua kiroho, kutumika, na kujenga umoja katika familia ya Penuel.
Idara ya Wanawake ya T.A.G Penuel Revival Temple ni huduma inayolenga kuwajenga wanawake kiroho, kimaadili, na kijamii ili wawe mashuhuda wema wa Yesu Kristo katika familia, kanisa, na jamii.
Umoja wa wanaume (Christian Men Fellowship) kwa ajili ya kujenga misingi ya kifamilia, uongozi, na nguzo za kiuchumi kanisani.
Kikundi cha kusimamia huduma ya uimbaji, ala za muziki, na kuongoza madhabahu wakati wa ibada za sifa.
Mtandao wa vijana wa Penuel unaolenga kujenga maisha ya ujana yenye utakatifu, ubunifu, na mafanikio ya kimaisha.
Idara inayojikita katika kuwafundisha watoto Neno la Mungu na kuwalea katika misingi ya imani ya Kikristo tangu wakiwa wadogo.